Zaburi 141:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kama kupasua kuni na kuzichanja juu ya nchi, Ndivyo ilivyo mifupa yetu mdomoni pa kuzimu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mifupa yao itatawanywa mdomoni pa Kuzimu kama kuni zilizopasuliwa vipandevipande! Biblia Habari Njema - BHND Mifupa yao itatawanywa mdomoni pa Kuzimu kama kuni zilizopasuliwa vipandevipande! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mifupa yao itatawanywa mdomoni pa Kuzimu kama kuni zilizopasuliwa vipandevipande! Neno: Bibilia Takatifu Watasema, “Kama mtu anavyolima na kuvunja ardhi, ndivyo mifupa yetu imetawanywa kwenye mlango wa kaburi.” Neno: Maandiko Matakatifu Watasema, “Kama mtu anavyolima na kuvunja ardhi, ndivyo mifupa yetu imetawanywa kwenye mlango wa kaburi.” BIBLIA KISWAHILI Kama kupasua kuni na kuzichanja juu ya nchi, Ndivyo ilivyo mifupa yetu mdomoni pa kuzimu. |
Hapo waliingiwa na hofu pasipokuwapo hofu, Maana Mungu ameitawanya mifupa yake aliyekuhusuru. Umewatia aibu, Kwa sababu MUNGU amewadharau.
Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.
Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu ili tusijitumainie nafsi zetu, bali tumtumaini Mungu, awafufuaye wafu,
walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizungukazunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya;