Zaburi 140:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hakika wenye haki watalishukuru jina lako, Wenye adili watakaa mahali ulipo Wewe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hakika waadilifu watalisifu jina lako; wanyofu watakaa kwako. Biblia Habari Njema - BHND Hakika waadilifu watalisifu jina lako; wanyofu watakaa kwako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hakika waadilifu watalisifu jina lako; wanyofu watakaa kwako. Neno: Bibilia Takatifu Hakika wenye haki watalisifu jina lako, na waadilifu wataishi mbele zako. Neno: Maandiko Matakatifu Hakika wenye haki watalisifu jina lako, na waadilifu wataishi mbele zako. BIBLIA KISWAHILI Hakika wenye haki watalishukuru jina lako, Wenye adili watakaa mahali ulipo Wewe. |
Kwa kuwa BWANA ni mwenye haki, Apenda matendo ya haki, Wanyofu wa moyo watauona uso wake.
Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako kuna furaha tele; Na katika mkono wako wa kulia Mna mema ya milele.
Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.
Mfurahieni BWANA; Shangilieni, enyi wenye haki Pigeni vigelegele vya furaha; Ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo.
Mifupa yangu yote itasema, BWANA, ni nani aliye kama Wewe? Umponyaye maskini kutoka kwa mtu aliye hodari kumshinda yeye, Naam, maskini na mhitaji na mtu amtekaye.
Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo.
Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu.
Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.