Ndipo BWANA akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto kutoka mbinguni kwa BWANA.
Zaburi 140:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Makaa ya moto yawaangukie, watupwe motoni, Na katika mashimo, wasipate kusimama tena. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Makaa ya moto yawaangukie; watumbukizwe mashimoni, wasiinuke tena. Biblia Habari Njema - BHND Makaa ya moto yawaangukie; watumbukizwe mashimoni, wasiinuke tena. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Makaa ya moto yawaangukie; watumbukizwe mashimoni, wasiinuke tena. Neno: Bibilia Takatifu Makaa ya mawe ya moto na yawaangukie! Na watupwe motoni, katika mashimo ya matope, wasiinuke tena kamwe. Neno: Maandiko Matakatifu Makaa ya mawe ya moto na yawaangukie! Na watupwe motoni, katika mashimo ya matope, wasiinuke tena kamwe. BIBLIA KISWAHILI Makaa ya moto yawaangukie, watupwe motoni, Na katika mashimo, wasipate kusimama tena. |
Ndipo BWANA akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto kutoka mbinguni kwa BWANA.
Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na kiberiti na upepo wa joto Na viwe fungu la kikombe chao.
Utawafanya kuwa kama tanuri ya moto, Wakati wa ghadhabu yako. BWANA atawameza kwa ghadhabu yake, Na moto utawateketeza.
Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.
Kila mtu awapotezaye wenye haki katika njia mbaya, Ataanguka katika rima lake mwenyewe; Bali wakamilifu watarithi mema.
Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.