Zaburi 14:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye hekima, Amtafutaye Mungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu anawaangalia wanadamu kutoka mbinguni, aone kama kuna yeyote mwenye busara, kama kuna yeyote anayemtafuta Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu anawaangalia wanadamu kutoka mbinguni, aone kama kuna yeyote mwenye busara, kama kuna yeyote anayemtafuta Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu anawaangalia wanadamu kutoka mbinguni, aone kama kuna yeyote mwenye busara, kama kuna yeyote anayemtafuta Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu anawachungulia wanadamu kutoka mbinguni aone kama kuna mwenye hekima, yeyote anayemtafuta Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu bwana anawachungulia wanadamu chini kutoka mbinguni aone kama wako wenye akili, wowote wanaomtafuta Mungu. BIBLIA KISWAHILI Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye hekima, Amtafutaye Mungu. |
basi, nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua.
Walakini, yameonekana kiasi cha mema ndani yako, kwa kuwa umeyaondoa Maashera katika nchi, na moyo wako umeukaza kumtafuta Mungu.
aukazaye moyo wake kumtafuta Mungu, BWANA, Mungu wa babaze, hata ikiwa si kwa utakaso wa patakatifu.
Je! Mwanadamu ni kitu gani, hata akawa safi? Huyo aliyezaliwa na mwanamke, hata awe na haki?
BWANA yu katika hekalu lake takatifu. BWANA ambaye kiti chake kiko mbinguni, Macho yake yanaangalia; Kope zake zinawapima wanadamu.
Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe.
Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zimezuiliwa kwangu.
Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong'ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?
Kwa maana watu wangu ni wapumbavu, hawanijui; ni watoto waliopungukiwa na akili, wala hawana ufahamu; ni wenye akili katika kutenda mabaya, bali katika kutenda mema hawana maarifa.
Pigeni mbio huku na huku katika njia za Yerusalemu, mkaone sasa, na kujua, na kutafuta katika viwanja vyake, kwamba mwaweza kumpata mtu mmoja, kwamba yuko mtu mmoja awaye yote atendaye kwa haki, atafutaye uaminifu; nami nitausamehe mji huo.
Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika; bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa.
Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.