Zaburi 139:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uangalie kama mwenendo wangu ni mbaya, uniongoze katika njia ya milele. Biblia Habari Njema - BHND Uangalie kama mwenendo wangu ni mbaya, uniongoze katika njia ya milele. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uangalie kama mwenendo wangu ni mbaya, uniongoze katika njia ya milele. Neno: Bibilia Takatifu Uone kama kuna njia iletayo machukizo ndani yangu, uniongoze katika njia ya milele. Neno: Maandiko Matakatifu Uone kama kuna njia iletayo machukizo ndani yangu, uniongoze katika njia ya milele. BIBLIA KISWAHILI Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele. |
Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, Kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze katika njia iliyo sawa,
Uniwezeshe kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unifundishe njia nitakayoiendea, Kwa maana ninakuinulia nafsi yangu.
Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako kuna furaha tele; Na katika mkono wako wa kulia Mna mema ya milele.
Umenijaribu moyo wangu, umenijia usiku, Umenichunguza usione neno; Nimenuia kinywa changu kisikose,
Ee BWANA, unifundishe njia yako, Na kuniongoza katika njia iliyonyoka; Kwa sababu yao wanaoniotea;
BWANA, uniongoze kwa haki yako, Kwa sababu yao wanaoniotea. Uinyoshe njia yako mbele ya uso wangu,
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.