Akaondoka kati ya usiku, akamwondoa mtoto wangu ubavuni pangu, mimi mjakazi wako nilipokuwa usingizini, akamweka kifuani pake, na mtoto wake mwenyewe, aliyekuwa amekufa, akamweka kifuani pangu.
Zaburi 139:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama ningeliomba giza linifunike, giza linizunguke badala ya mwanga, Biblia Habari Njema - BHND Kama ningeliomba giza linifunike, giza linizunguke badala ya mwanga, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama ningeliomba giza linifunike, giza linizunguke badala ya mwanga, Neno: Bibilia Takatifu Nikisema, “Hakika giza litanificha na nuru inayonizunguka iwe usiku,” Neno: Maandiko Matakatifu Kama nikisema, “Hakika giza litanificha na nuru inayonizunguka iwe usiku,” BIBLIA KISWAHILI Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku; |
Akaondoka kati ya usiku, akamwondoa mtoto wangu ubavuni pangu, mimi mjakazi wako nilipokuwa usingizini, akamweka kifuani pake, na mtoto wake mwenyewe, aliyekuwa amekufa, akamweka kifuani pangu.
Ole wao wanaojitahidi kumficha BWANA mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye?
Je, mtu yeyote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema BWANA. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema BWANA.