Zaburi 138:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ee BWANA, wafalme wote wa dunia watakushukuru, Watakapoyasikia maneno ya kinywa chako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wafalme wote duniani watakusifu, ee Mwenyezi-Mungu, kwa sababu wameyasikia maneno yako. Biblia Habari Njema - BHND Wafalme wote duniani watakusifu, ee Mwenyezi-Mungu, kwa sababu wameyasikia maneno yako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wafalme wote duniani watakusifu, ee Mwenyezi-Mungu, kwa sababu wameyasikia maneno yako. Neno: Bibilia Takatifu Wafalme wote wa dunia wakusifu wewe Ee Mwenyezi Mungu, wakati wanaposikia maneno ya kinywa chako. Neno: Maandiko Matakatifu Wafalme wote wa dunia wakusifu wewe Ee bwana, wakati wanaposikia maneno ya kinywa chako. BIBLIA KISWAHILI Ee BWANA, wafalme wote wa dunia watakushukuru, Watakapoyasikia maneno ya kinywa chako. |
Miisho yote ya dunia itakumbuka, Na watu watamrejea BWANA; Jamaa zote za mataifa watamsujudia.
Na hata nikiwa ni mzee mwenye mvi, Ee Mungu, usiniache. Hata niwaeleze watu wa kizazi hiki nguvu zako, Na kila atakayekuja uweza wako.
Na wafalme watakuwa baba zako walezi, na malkia zao mama zako walezi; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni BWANA, tena waningojeao hawatatahayarika.
Utanyonya maziwa ya mataifa, Utanyonya matiti ya wafalme; Nawe utajua ya kuwa mimi, BWANA, ni mwokozi wako, Na mkombozi wako, Mwenye enzi wa Yakobo.
Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.
Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.