Kwa sababu hiyo ukawatia katika mikono ya adui zao, waliowasumbua; na wakati wa shida yao, walipokulilia, uliwasikia kutoka mbinguni; na kwa wingi wa rehema zako ukawapa waokozi waliowaokoa kutoka mikononi mwa adui zao.
Zaburi 136:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akatuokoa na watesi wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema akatuokoa kutoka maadui zetu; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Biblia Habari Njema - BHND akatuokoa kutoka maadui zetu; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza akatuokoa kutoka maadui zetu; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Neno: Bibilia Takatifu Alituweka huru toka adui zetu, Fadhili zake zadumu milele. Neno: Maandiko Matakatifu Alituweka huru toka adui zetu, Fadhili zake zadumu milele. BIBLIA KISWAHILI Akatuokoa na watesi wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
Kwa sababu hiyo ukawatia katika mikono ya adui zao, waliowasumbua; na wakati wa shida yao, walipokulilia, uliwasikia kutoka mbinguni; na kwa wingi wa rehema zako ukawapa waokozi waliowaokoa kutoka mikononi mwa adui zao.
Wewe kwa rehema zako umewaongoza watu uliowakomboa, Kwa uweza wako uliwaelekeza hata makao yako matakatifu.
Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale.
Nawe kumbuka kwamba ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, akakukomboa BWANA, Mungu wako; kwa hiyo mimi nakuamuru neno hili hivi leo.
ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wake mwenyewe walio na bidii katika matendo mema.