Nayo nyumba nitakayoijenga ni kubwa; kwa sababu Mungu wetu ndiye mkuu juu ya miungu yote.
Zaburi 136:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mshukuruni Mungu wa miungu; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Biblia Habari Njema - BHND Mshukuruni Mungu wa miungu; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mshukuruni Mungu wa miungu; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Neno: Bibilia Takatifu Mshukuruni Mungu wa miungu. Fadhili zake zadumu milele. Neno: Maandiko Matakatifu Mshukuruni Mungu wa miungu. Fadhili zake zadumu milele. BIBLIA KISWAHILI Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. |
Nayo nyumba nitakayoijenga ni kubwa; kwa sababu Mungu wetu ndiye mkuu juu ya miungu yote.
Na waaibishwe wote waabuduo sanamu, Wajivunao kwa vitu visivyofaa; Enyi miungu yote, msujuduni Yeye.
Maana Wewe, BWANA, ndiwe Uliye juu, Juu sana kuliko nchi yote; Umetukuka sana juu ya miungu yote.
Sasa najua ya kuwa BWANA ni mkuu kuliko miungu yote; naam, katika jambo hilo walilowatenda kwa ujeuri.
Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, Hakika Mungu wenu ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme, awezaye kufumbua siri, kwa kuwa wewe uliweza kuifumbua siri hii.
Kwa maana BWANA, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea watu, wala kukubali rushwa.
Mungu, Mungu BWANA, naam, Mungu, Mungu BWANA, yeye anajua, na Israeli naye atajua; kama ni katika uasi, au kama ni katika kosa juu ya BWANA, usituokoe hivi leo;