Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Zaburi 136:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Akawaondoa watu wa Israeli kutoka huko; kwa maana fadhili zake zadumu milele.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Akawaondoa watu wa Israeli kutoka huko; kwa maana fadhili zake zadumu milele.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Akawaondoa watu wa Israeli kutoka huko; kwa maana fadhili zake zadumu milele.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Na kuwatoa Israeli katikati yao, Fadhili zake zadumu milele.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Na kuwatoa Israeli katikati yao, Fadhili zake zadumu milele.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Zaburi 136:11
11 Marejeleo ya Msalaba  

Akawatoa wakiwa na fedha na dhahabu, Katika makabila yao asiwepo mwenye kujikwaa.


Kisha akawaongoza watu wake kama kondoo, Akawachunga kama kundi jangwani.


Ilikuwa mwisho wa miaka hiyo mia nne na thelathini, ilikuwa siku ile ile, majeshi yote ya BWANA yalitoka nchi ya Misri.


Ni usiku wa kuangaliwa sana mbele za BWANA kwa sababu ya kuwatoa katika nchi ya Misri; huu ndio usiku wa BWANA, ambao wapasa kuangaliwa sana na wana wa Israeli wote katika vizazi vyao.


Ilikuwa siku ile ile moja, BWANA akawatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri kwa majeshi yao.


Kisha itakuwa hapo mwanao atakapokuuliza kesho, akisema, Ni nini hivi? Utamwambia, BWANA alimtoa Misri, kutoka ile nyumba ya utumwa, kwa uwezo wa mkono wake;


Jambo hilo litakuwa ni ishara mkononi mwako, na utepe katikati ya macho yako; kwa kuwa BWANA alitutoa Misri kwa uwezo wa mkono wake.


Ilikuwa hapo Farao alipowaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije wakabadili nia watu hawa hapo watakapokumbana na vita, na kurudi Misri;


Musa akawaambia hao watu, Kumbukeni siku hii, mliyotoka nchi ya Misri, kutoka nyumba ya utumwa; kwa kuwa BWANA aliwatoa mahali hapa kwa nguvu za mkono wake; na usiliwe mkate uliochachwa.


Nayo itakuwa ishara kwako katika mkono wako, na kwa ukumbusho kati ya macho yako, ili kwamba sheria ya BWANA ipate kuwa kinywani mwako; kwani BWANA alikuondoa utoke Misri kwa mkono wenye uwezo.