Zaburi 135:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ninyi msimamao nyumbani mwa BWANA, Nyuani mwa nyumba ya Mungu wenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Msifuni enyi mkaao katika nyumba yake, ukumbini mwa nyumba ya Mungu wetu! Biblia Habari Njema - BHND Msifuni enyi mkaao katika nyumba yake, ukumbini mwa nyumba ya Mungu wetu! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Msifuni enyi mkaao katika nyumba yake, ukumbini mwa nyumba ya Mungu wetu! Neno: Bibilia Takatifu ninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu, katika nyua za nyumba ya Mungu wetu. Neno: Maandiko Matakatifu ninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba ya bwana, katika nyua za nyumba ya Mungu wetu. BIBLIA KISWAHILI Ninyi msimamao nyumbani mwa BWANA, Nyuani mwa nyumba ya Mungu wenu. |
Mkasimame katika patakatifu, kama ndugu zenu wana wa watu walivyogawanyika kufuata nyumba za mababa, kadiri ya mgawanyiko wa kila nyumba ya baba, ya Walawi.
Ndipo Walawi, Yeshua na Kadmieli, na Bani, na Hashabneya, na Sherebia, na Hodia, na Shebania, na Pethahia, wakasema, Simameni, mkamhimidi BWANA, Mungu wenu, tangu milele na hata milele. Na lihimidiwe jina lako tukufu, lililotukuka kuliko baraka zote na sifa zote.
Njoni, enyi watumishi wote wa BWANA, Mhimidini BWANA Ninyi mnaohudumu usiku Katika nyumba ya BWANA.
Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.