Ezra akamhimidi BWANA, Mungu Mkuu. Nao watu wote wakaitika, Amina, Amina, pamoja na kuinua mikono yao; kisha wakainamisha vichwa vyao, wakamsujudu BWANA kifudifudi.
Zaburi 134:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Painulieni patakatifu mikono yenu, Na kumhimidi BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Inueni mikono kuelekea mahali patakatifu, na kumtukuza Mwenyezi-Mungu! Biblia Habari Njema - BHND Inueni mikono kuelekea mahali patakatifu, na kumtukuza Mwenyezi-Mungu! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Inueni mikono kuelekea mahali patakatifu, na kumtukuza Mwenyezi-Mungu! Neno: Bibilia Takatifu Inueni mikono yenu katika patakatifu na kumsifu Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Inueni mikono yenu katika pale patakatifu na kumsifu bwana. BIBLIA KISWAHILI Painulieni patakatifu mikono yenu, Na kumhimidi BWANA. |
Ezra akamhimidi BWANA, Mungu Mkuu. Nao watu wote wakaitika, Amina, Amina, pamoja na kuinua mikono yao; kisha wakainamisha vichwa vyao, wakamsujudu BWANA kifudifudi.
Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.
Inuka, ulalamike usiku, Mwanzo wa mikesha yake; Mimina moyo wako kama maji usoni pa Bwana; Umwinulie mikono yako; Kwa uhai wa watoto wako wachanga wazimiao kwa njaa, Mwanzo wa kila njia kuu.
Basi, nataka wanaume waombe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano.