Abramu akamwambia Lutu, Basi, usiwepo ugomvi, nakusihi, kati yangu na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wachungaji wako; maana sisi tu jamaa moja.
Zaburi 133:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tazama, jinsi ilivyo vyema, na kupendeza, Ndugu kuishi pamoja, kwa umoja. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ni jambo zuri na la kupendeza sana ndugu kuishi pamoja kwa umoja. Biblia Habari Njema - BHND Ni jambo zuri na la kupendeza sana ndugu kuishi pamoja kwa umoja. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ni jambo zuri na la kupendeza sana ndugu kuishi pamoja kwa umoja. Neno: Bibilia Takatifu Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza ndugu wanapoishi pamoja katika umoja! Neno: Maandiko Matakatifu Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza wakati ndugu wanapoishi pamoja katika umoja! BIBLIA KISWAHILI Tazama, jinsi ilivyo vyema, na kupendeza, Ndugu kuishi pamoja, kwa umoja. |
Abramu akamwambia Lutu, Basi, usiwepo ugomvi, nakusihi, kati yangu na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wachungaji wako; maana sisi tu jamaa moja.
BWANA, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala mambo yanayozidi nguvu zangu.
Na wivu wa Efraimu utaondoka, na wale wanaomwudhi Yuda watakatiliwa mbali; Efraimu hatamhusudu Yuda, wala Yuda hatamwudhi Efraimu.
Mbwamwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwanasimba na ng'ombe wanono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza.
Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua BWANA, kama vile maji yanavyoifunika bahari.
nami nitawapa moyo mmoja na njia moja, wapate kunicha sikuzote; kwa mema yao, na ya watoto wao baada yao;
Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.
Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu migawanyiko, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.
Neno la mwisho ni hili; muwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;