Zaburi 132:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na tuingie katika maskani yake, Tusujudu penye kiti cha kuwekea miguu yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Haya! Twende nyumbani kwa Mungu, tuabudu mbele ya kiti chake cha enzi!” Biblia Habari Njema - BHND “Haya! Twende nyumbani kwa Mungu, tuabudu mbele ya kiti chake cha enzi!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Haya! Twende nyumbani kwa Mungu, tuabudu mbele ya kiti chake cha enzi!” Neno: Bibilia Takatifu “Twendeni kwenye makao yake, na tuabudu kwenye kiti cha kuwekea miguu yake; Neno: Maandiko Matakatifu “Twendeni kwenye makao yake, na tuabudu kwenye kiti cha kuwekea miguu yake; BIBLIA KISWAHILI Na tuingie katika maskani yake, Tusujudu penye kiti cha kuwekea miguu yake. |
Bali mimi, kwa wingi wa fadhili zako, Nitaingia nyumbani mwako; Na kusujudu kwa kicho, Nikilielekea hekalu lako takatifu.
Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu; Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu; Maana BWANA, Mungu wetu, ni mtakatifu.
Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa BWANA, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la BWANA katika Yerusalemu.
Jinsi Bwana alivyomfunika binti Sayuni Kwa wingu katika hasira yake! Ameutupa toka mbinguni hata nchi Huo uzuri wa Israeli; Wala hakukikumbuka kiti cha miguu yake Katika siku ya hasira yake.