Nami nitampa mwana wake kabila moja, ili Daudi, mtumishi wangu, apate kuwa na taa siku zote mbele zangu katika Yerusalemu, mji ule niliouchagua niweke jina langu huko.
Zaburi 132:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hapo nitamchipushia Daudi pembe, Na taa nimemtengenezea masihi wangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Humo nitamchipusha mfalme shujaa wa ukoo wa Daudi: Kama taa iwakayo nitamtegemeza mfalme niliyemteua. Biblia Habari Njema - BHND Humo nitamchipusha mfalme shujaa wa ukoo wa Daudi: Kama taa iwakayo nitamtegemeza mfalme niliyemteua. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Humo nitamchipusha mfalme shujaa wa ukoo wa Daudi: kama taa iwakayo nitamtegemeza mfalme niliyemteua. Neno: Bibilia Takatifu “Hapa nitamchipushia Daudi pembe, na kuweka taa kwa ajili ya masiya wangu. Neno: Maandiko Matakatifu “Hapa nitamchipushia Daudi pembe, na kuweka taa kwa ajili ya masiya wangu. BIBLIA KISWAHILI Hapo nitamchipushia Daudi pembe, Na taa nimemtengenezea masihi wangu. |
Nami nitampa mwana wake kabila moja, ili Daudi, mtumishi wangu, apate kuwa na taa siku zote mbele zangu katika Yerusalemu, mji ule niliouchagua niweke jina langu huko.
Lakini kwa ajili ya Daudi, BWANA, Mungu wake, akampa taa humo Yerusalemu, amwinue mwanawe baada yake, na kuufanya imara Yerusalemu;
Walakini BWANA hakupenda kuiharibu Yuda, kwa ajili ya Daudi mtumishi wake, kama alivyomwahidia akasema, kuwa atampa taa, yeye na wazao wake siku zote.
Walakini BWANA hakupenda kuiharibu nyumba ya Daudi, kwa sababu ya agano alilolifanya na Daudi, na kama alivyomwahidi kuwa atampa taa, yeye na wazao wake siku zote.
Naye amewainulia watu wake pembe, Sifa za watauwa wake wote; Wana wa Israeli, watu walio karibu naye. Haleluya.
Siku ile nitawachipushia nyumba ya Israeli pembe, nami nitakujalia kufumbua kinywa kati yao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Washindanao na BWANA watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; BWANA ataihukumu dunia yote; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake.