Zaburi 132:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hakika nitavibariki vyakula vyake Wahitaji wake nitawashibisha chakula. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nitaubariki sana mji wa Siyoni kwa mahitaji yake; nitawashibisha chakula maskini wake. Biblia Habari Njema - BHND Nitaubariki sana mji wa Siyoni kwa mahitaji yake; nitawashibisha chakula maskini wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nitaubariki sana mji wa Siyoni kwa mahitaji yake; nitawashibisha chakula maskini wake. Neno: Bibilia Takatifu Nitambariki kwa kumpa mahitaji tele: nitashibisha maskini wake kwa chakula. Neno: Maandiko Matakatifu Nitambariki kwa kumpa mahitaji tele: nitashibisha maskini wake kwa chakula. BIBLIA KISWAHILI Hakika nitavibariki vyakula vyake Wahitaji wake nitawashibisha chakula. |
Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.
Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma.
Nami nitaishibisha roho ya makuhani kwa unono, na watu wangu watashiba kwa wema wangu, asema BWANA.
Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamtosheki na vinywaji; mnajivika nguo lakini hampati joto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotobokatoboka.
Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha mbali. Ni kwa sababu gani? Asema BWANA wa majeshi. Ni kwa sababu yumba yangu imebaki kuwa gofu la nyumba, wakati ambapo kila mmoja wenu anakimbilia nyumbani kwake.
Kama hamtaki kusikia, na kama hamtaki kuitia moyoni, ili kulitukuza jina langu, asema BWANA wa majeshi, basi nitawaleteeni laana, nami nitazilaani baraka zenu; naam, nimekwisha kuzilaani, kwa sababu hamyatii haya moyoni.
na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba BWANA, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.