Lakini sitauondoa ufalme wote pia; nitampa mwana wako kabila moja, kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, na kwa ajili ya Yerusalemu niliouchagua.
Zaburi 132:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa kuwa BWANA ameichagua Sayuni, Ameitamani akae ndani yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu ameuchagua mji wa Siyoni, ametaka uwe makao yake: Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu ameuchagua mji wa Siyoni, ametaka uwe makao yake: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu ameuchagua mji wa Siyoni, ametaka uwe makao yake: Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana Mwenyezi Mungu ameichagua Sayuni, amepaonea shauku pawe maskani yake: Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana bwana ameichagua Sayuni, amepaonea shauku pawe maskani yake: BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa BWANA ameichagua Sayuni, Ameitamani akae ndani yake. |
Lakini sitauondoa ufalme wote pia; nitampa mwana wako kabila moja, kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, na kwa ajili ya Yerusalemu niliouchagua.
Maana sasa nimeichagua nyumba hii na kuitakasa, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko milele; yatakuwako na macho yangu, na moyo wangu daima.
Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, BWANA, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee mpaka Yerusalemu, ulioko Yuda, akaijenge nyumba ya BWANA, Mungu wa Israeli, (yeye ndiye Mungu), iliyoko Yerusalemu.
Enyi milima mirefu, kwani kuutazama kwa wivu Mlima alioutamani Mungu akae juu yake? Naam, BWANA atakaa juu yake milele.
Wajumbe wa taifa hilo waletewe jibu gani? Ya kuwa BWANA ameiweka misingi ya Sayuni, na ndani yake wale walioonewa katika watu wake watapata kimbilio kwake.
Bali ninyi mmeufikia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,