Zaburi 130:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nimemngoja BWANA, roho yangu imengoja, Na neno lake nimelitumainia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Namtumainia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote; nina imani sana na neno lake. Biblia Habari Njema - BHND Namtumainia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote; nina imani sana na neno lake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Namtumainia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote; nina imani sana na neno lake. Neno: Bibilia Takatifu Namngojea Mwenyezi Mungu, nafsi yangu inangojea, katika neno lake naweka tumaini langu. Neno: Maandiko Matakatifu Namngojea bwana, nafsi yangu inangojea, katika neno lake naweka tumaini langu. BIBLIA KISWAHILI Nimemngoja BWANA, roho yangu imengoja, Na neno lake nimelitumainia. |
Naam, katika njia ya hukumu zako Sisi tumekungoja, Ee BWANA; Shauku ya nafsi zetu inaelekea Jina lako na ukumbusho wako.
Kwa ajili ya hayo BWANA atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana BWANA ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao.
Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.
Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake.
ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;