Ee BWANA, Mungu wa Israeli, wewe ndiwe mwenye haki, maana sisi tumesalia, mabaki yaliyookoka, kama hivi leo; tazama, sisi tupo hapa wenye hatia mbele zako; maana hapana mtu awezaye kusimama mbele zako kwa sababu ya jambo hili.
Zaburi 130:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama, ee Mwenyezi-Mungu ungekumbuka maovu yetu nani, ee Bwana, angeweza kusalimika? Biblia Habari Njema - BHND Kama, ee Mwenyezi-Mungu ungekumbuka maovu yetu nani, ee Bwana, angeweza kusalimika? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama, ee Mwenyezi-Mungu ungekumbuka maovu yetu nani, ee Bwana, angeweza kusalimika? Neno: Bibilia Takatifu Kama wewe, Ee Mwenyezi Mungu, ungeweka kumbukumbu ya dhambi, Ee Bwana, ni nani angeweza kusimama? Neno: Maandiko Matakatifu Kama wewe, Ee bwana, ungeweka kumbukumbu ya dhambi, Ee Bwana, ni nani angeliweza kusimama? BIBLIA KISWAHILI BWANA, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? |
Ee BWANA, Mungu wa Israeli, wewe ndiwe mwenye haki, maana sisi tumesalia, mabaki yaliyookoka, kama hivi leo; tazama, sisi tupo hapa wenye hatia mbele zako; maana hapana mtu awezaye kusimama mbele zako kwa sababu ya jambo hili.
Je! Mwanadamu ni kitu gani, hata akawa safi? Huyo aliyezaliwa na mwanamke, hata awe na haki?
Ingawa mimi ni mwenye haki, kinywa changu mwenyewe kitanihukumu; Ingawa mimi ni mkamilifu, kitanishuhudia kuwa mimi ni mpotovu.
Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na BWANA ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.
Ni nani awezaye kusimama mbele za ghadhabu yake, naye ni nani awezaye kukaa katika ukali wa hasira yake? Hasira yake kali humwagwa kama moto, nayo majabali yapasuliwa na yeye.
Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo;
Wakumbuke watumishi wako, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; usiangalie ukaidi wa watu hawa, wala uovu wao, wala dhambi yao;