Na sasa, Ee Mungu wangu, macho yako yafumbuke, nakusihi, masikio yako yakasikilize maombi yaombwayo mahali hapa.
Zaburi 130:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Bwana, uisikie sauti yangu. Masikio yako na yaisikilize Sauti ya dua zangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ee Bwana, sikia sauti yangu, uitegee sikio sauti ya ombi langu. Biblia Habari Njema - BHND Ee Bwana, sikia sauti yangu, uitegee sikio sauti ya ombi langu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ee Bwana, sikia sauti yangu, uitegee sikio sauti ya ombi langu. Neno: Bibilia Takatifu Ee Bwana, sikia sauti yangu. Masikio yako na yawe masikivu kwa kilio changu unihurumie. Neno: Maandiko Matakatifu Ee bwana, sikia sauti yangu. Masikio yako na yawe masikivu kwa kilio changu unihurumie. BIBLIA KISWAHILI Bwana, uisikie sauti yangu. Masikio yako na yaisikilize Sauti ya dua zangu. |
Na sasa, Ee Mungu wangu, macho yako yafumbuke, nakusihi, masikio yako yakasikilize maombi yaombwayo mahali hapa.
Ee Bwana, nakusihi, litege sikio lako, uyasikilize maombi ya mtumishi wako, na maombi ya watumishi wako, wanaofurahi kulicha jina lako; nakuomba sana; unifanikishe mimi, mtumishi wako, leo, ukanijalie rehema mbele ya mtu huyu. (Maana, nilikuwa mnyweshaji wa mfalme).
tega sikio lako, macho yako yakafumbuke, upate kuyasikiliza maombi ya mtumishi wako, ninayoomba mbele zako wakati huu, mchana na usiku, kwa ajili ya wana wa Israeli, watumishi wako; hapo ninapoziungama dhambi za wana wa Israeli, tulizozifanya juu yako; naam, mimi na nyumba ya baba yangu tumefanya dhambi.
Ee BWANA, usikie haki, ukisikilize kilio changu, Utege sikio lako kwa maombi yangu, Yasiyotoka katika midomo ya hila.
Mungu, uisikie sauti yangu katika malalamiko yangu; Unilinde uhai wangu kutoka kwa hofu ya adui.
Tega sikio lako, BWANA, usikie; funua macho yako, BWANA, uone; uyasikie maneno ya Senakeribu, aliyopeleka ili kumtukana Mungu aliye hai.