Na sasa kwa muda kidogo tumeneemeshwa na BWANA, Mungu wetu, hata akatuachia mabaki yaokoke, akatupa msumari katika mahali pake patakatifu. Mungu wetu atutie nuru machoni mwetu, tuburudike kidogo katika kufungwa kwetu.
Zaburi 13:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Adui yangu asije akasema, Nimemshinda; Watesi wangu wasifurahi ninapoondoshwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usiwaache maadui zangu waseme: “Tumemweza huyu!” Watesi wangu wasije wakafurahia kuanguka kwangu. Biblia Habari Njema - BHND Usiwaache maadui zangu waseme: “Tumemweza huyu!” Watesi wangu wasije wakafurahia kuanguka kwangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usiwaache maadui zangu waseme: “Tumemweza huyu!” Watesi wangu wasije wakafurahia kuanguka kwangu. Neno: Bibilia Takatifu Adui yangu atasema, “Nimemshinda,” nao adui zangu watashangilia nitakapoanguka. Neno: Maandiko Matakatifu Adui yangu atasema, “Nimemshinda,” nao adui zangu watashangilia nitakapoanguka. BIBLIA KISWAHILI Adui yangu asije akasema, Nimemshinda; Watesi wangu wasifurahi ninapoondoshwa. |
Na sasa kwa muda kidogo tumeneemeshwa na BWANA, Mungu wetu, hata akatuachia mabaki yaokoke, akatupa msumari katika mahali pake patakatifu. Mungu wetu atutie nuru machoni mwetu, tuburudike kidogo katika kufungwa kwetu.
Maana nilisema, Wasije wakanifurahia; Wale wanaojitukuza juu yangu Mguu wangu unapoteleza.
Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema BWANA, ili nikuokoe.
Mimi ninayalilia mambo hayo; Jicho langu, jicho langu linachuruzika machozi; Kwa kuwa mfariji yuko mbali nami, Ambaye ilimpasa kunihuisha nafsi; Watoto wangu wameachwa peke yao, Kwa sababu huyo adui ameshinda.
Maana Wakanaani na wenyeji wote wa nchi hii watasikia habari hii, nao watatuzingira, na kulifuta jina letu katika nchi. Nawe utafanya nini kwa ajili ya jina lako kuu?