Na sasa kwa muda kidogo tumeneemeshwa na BWANA, Mungu wetu, hata akatuachia mabaki yaokoke, akatupa msumari katika mahali pake patakatifu. Mungu wetu atutie nuru machoni mwetu, tuburudike kidogo katika kufungwa kwetu.
Zaburi 13:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie; Uyatie nuru macho yangu, Nisije nikalala usingizi wa mauti. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uniangalie na kunijibu, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu. Uyaangazie macho yangu, nisipatwe na usingizi wa kifo. Biblia Habari Njema - BHND Uniangalie na kunijibu, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu. Uyaangazie macho yangu, nisipatwe na usingizi wa kifo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uniangalie na kunijibu, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu. Uyaangazie macho yangu, nisipatwe na usingizi wa kifo. Neno: Bibilia Takatifu Nitazame, unijibu, Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu. Yatie nuru macho yangu, ama sivyo nitalala usingizi wa mauti. Neno: Maandiko Matakatifu Nitazame, unijibu, Ee bwana Mwenyezi Mungu wangu. Yatie nuru macho yangu, ama sivyo nitalala usingizi wa mauti. BIBLIA KISWAHILI Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie; Uyatie nuru macho yangu, Nisije nikalala usingizi wa mauti. |
Na sasa kwa muda kidogo tumeneemeshwa na BWANA, Mungu wetu, hata akatuachia mabaki yaokoke, akatupa msumari katika mahali pake patakatifu. Mungu wetu atutie nuru machoni mwetu, tuburudike kidogo katika kufungwa kwetu.
Na nishangilie, nizifurahie fadhili zako, Kwa kuwa umeyaona mateso yangu. Umeijua nafsi yangu taabuni,
Wewe, BWANA, unifadhili, Tazama mateso niteswayo na wanaonichukia; Wewe uniinuaye katika malango ya mauti,
Wakiingiwa na ukali, nitawafanyia karamu yao, nami nitawalevya, wapate kufurahi, na kulala usingizi wa milele, wasiamke tena, asema BWANA.
Nami nitawalevya wakuu wake, na watu wake wenye hekima, watawala wake, na makamanda wake, na mashujaa wake; nao watalala usingizi wa milele, wasiamke, asema Mfalme, BWANA wa majeshi, ambaye jina lake ni BWANA.
Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-kondoo.
Ila Yonathani hakusikia, hapo babaye alipowaagiza watu kwa kiapo; basi yeye akainyosha ncha ya fimbo iliyokuwa mkononi mwake, na kuichovya katika sega la asali, kisha akatia mkono wake kinywani; na macho yake yakatiwa nuru.
Ndipo Yonathani akasema, Babangu ameifadhaisha nchi; tafadhali, angalia jinsi macho yangu yalivyotiwa nuru, kwa sababu nilionja asali hii kidogo.