Basi mfalme akaniambia, Mbona umesikitika uso wako, nawe huna ugonjwa? Nini hii, isipokuwa ni huzuni ya moyo? Ndipo nikaogopa sana.
Zaburi 13:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nitakuwa na wasiwasi rohoni mwangu hadi lini, Nikihuzunika moyoni mchana kutwa? Adui yangu atatukuka juu yangu hadi lini? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nitakuwa na wasiwasi rohoni hadi lini, na sikitiko moyoni siku hata siku? Hadi lini adui zangu watafurahia taabu zangu? Biblia Habari Njema - BHND Nitakuwa na wasiwasi rohoni hadi lini, na sikitiko moyoni siku hata siku? Hadi lini adui zangu watafurahia taabu zangu? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nitakuwa na wasiwasi rohoni hadi lini, na sikitiko moyoni siku hata siku? Hadi lini adui zangu watafurahia taabu zangu? Neno: Bibilia Takatifu Nitapambana na mawazo yangu hadi lini, na kila siku kuwa na majonzi moyoni mwangu? Adui zangu watanishinda hadi lini? Neno: Maandiko Matakatifu Nitapambana na mawazo yangu mpaka lini, na kila siku kuwa na majonzi moyoni mwangu? Adui zangu watanishinda mpaka lini? BIBLIA KISWAHILI Nitakuwa na wasiwasi rohoni mwangu hadi lini, Nikihuzunika moyoni mchana kutwa? Adui yangu atatukuka juu yangu hadi lini? |
Basi mfalme akaniambia, Mbona umesikitika uso wako, nawe huna ugonjwa? Nini hii, isipokuwa ni huzuni ya moyo? Ndipo nikaogopa sana.
Esta akasema, Ni mtesi, tena ni adui, ndiye huyu Hamani, mtu mbaya kabisa. Mara Hamani akaingiwa na hofu mbele ya mfalme na malkia.
Mimi nikiwa mwovu, ole wangu! Nami nikiwa mwenye haki, walakini sitainua kichwa changu; Maana nimejaa aibu Nikiyaangalia mateso yangu.
Midomo ya uongo iwe na ububu, Imneneayo mwenye haki maneno ya kiburi, Kwa majivuno na dharau.
Nayakumbuka mambo haya kwa uchungu moyoni mwangu, Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano, Na kuwaongoza hadi katika nyumba ya Mungu, Kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu.
Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao Umeiweka misingi ya nguvu; Kwa sababu yao wanaoshindana nawe; Uwakomeshe adui na mjilipiza kisasi.
Adui wameangamia na kuwa magofu milele. Nayo miji yao uliing'oa; Hata kumbukumbu lao limepotea.
Mbona maumivu yangu ni ya daima, na jeraha langu halina dawa, linakataa kuponywa? Je! Yamkini wewe utakuwa kwangu kama kijito kidanganyacho, na kama maji yasiyodumu?
Ulisema, Ole wangu! Kwa maana BWANA ameongeza huzuni pamoja na maumivu yangu. Nimechoka kwa ajili ya kuugua kwangu, wala sioni raha.
Watesi wake wamekuwa kichwa, Adui zake hufanikiwa; Kwa kuwa BWANA amemtesa Kwa sababu ya wingi wa makosa yake; Watoto wake wadogo wamechukuliwa mateka Mbele yake huyo mtesi.
Uchafu wake ulikuwa katika marinda yake; Hakukumbuka mwisho wake; Kwa hiyo ameshuka kwa ajabu; Yeye hana mtu wa kumfariji; Tazama, BWANA, mateso yangu; Maana huyo adui amejitukuza.
Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami.
Kila siku nilipokuwa pamoja nanyi hekaluni hamkuninyoshea mikono, lakini hii ndiyo saa yenu, na mamlaka ya giza.
Kwa maana alikuwa mgonjwa sana, karibu kufa; lakini Mungu alimhurumia; wala si yeye peke yake, ila na mimi pia; nisiwe na huzuni juu ya huzuni.
Naye Sauli akazidi kumwogopa Daudi; tangu wakati huo, Sauli akawa adui yake Daudi daima.
Maana mtu akimwona adui yake, je! Atamwacha aende zake salama? Basi BWANA na akulipe mema kwa haya uliyonitendea leo.