Na tazama, masuke saba membamba, dhaifu, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao.
Zaburi 129:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na wawe kama majani ya darini Yanyaukayo kabla hayajamea. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wawe kama nyasi juu ya paa la nyumba, ambazo hunyauka kabla hazijakua, Biblia Habari Njema - BHND Wawe kama nyasi juu ya paa la nyumba, ambazo hunyauka kabla hazijakua, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wawe kama nyasi juu ya paa la nyumba, ambazo hunyauka kabla hazijakua, Neno: Bibilia Takatifu Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua; Neno: Maandiko Matakatifu Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua; BIBLIA KISWAHILI Na wawe kama majani ya darini Yanyaukayo kabla hayajamea. |
Na tazama, masuke saba membamba, dhaifu, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao.
Ndiyo sababu wenyeji wao walikuwa na nguvu chache, wakafadhaika, na kuhangaika; wakawa kama majani ya mashamba, kama miche mibichi, kama majani juu ya dari, na kama ngano iliyokaushwa kabla haijaiva.
Hata wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakastawi. Mwishowe wataangamizwa milele;
Ndiyo sababu wenyeji wao wakawa hawana nguvu, na kufadhaika, na kuhangaika, wakawa kama majani ya mashamba, kama miche mibichi, kama majani juu ya madari, kama shamba la ngano kabla haijaiva.