Ee BWANA, Mungu wa Israeli, wewe ndiwe mwenye haki, maana sisi tumesalia, mabaki yaliyookoka, kama hivi leo; tazama, sisi tupo hapa wenye hatia mbele zako; maana hapana mtu awezaye kusimama mbele zako kwa sababu ya jambo hili.
Zaburi 129:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA ndiye mwenye haki, Amezikata kamba zao wasio haki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu; amezikata kamba za hao watu waovu.” Biblia Habari Njema - BHND Lakini Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu; amezikata kamba za hao watu waovu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu; amezikata kamba za hao watu waovu.” Neno: Bibilia Takatifu Lakini Mwenyezi Mungu ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini bwana ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu. BIBLIA KISWAHILI BWANA ndiye mwenye haki, Amezikata kamba zao wasio haki. |
Ee BWANA, Mungu wa Israeli, wewe ndiwe mwenye haki, maana sisi tumesalia, mabaki yaliyookoka, kama hivi leo; tazama, sisi tupo hapa wenye hatia mbele zako; maana hapana mtu awezaye kusimama mbele zako kwa sababu ya jambo hili.
Lakini wewe u mwenye haki, katika hayo yote yaliyotupata; maana wewe umetenda yaliyo kweli, lakini sisi tumetenda yaliyo maovu;
BWANA ndiye mwenye haki; Maana nimeiasi amri yake; Sikieni, nawasihi, enyi watu wote, Mkayatazame majonzi yangu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wamechukuliwa mateka.
Ee Bwana, haki ina wewe, lakini kwetu sisi kuna aibu, kama hivi leo; kwa watu wa Yuda, na kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa Israeli wote, walio karibu na hao walio mbali, katika nchi zote ulikowafukuza, kwa sababu ya makosa yao waliyokukosa.