Zaburi 129:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Lakini hawakuniweza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu, lakini hawakufaulu kunishinda. Biblia Habari Njema - BHND “Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu, lakini hawakufaulu kunishinda. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu, lakini hawakufaulu kunishinda. Neno: Bibilia Takatifu wamenitesa sana tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda. Neno: Maandiko Matakatifu wamenionea mno tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda. BIBLIA KISWAHILI Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Lakini hawakuniweza. |
Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu.
Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.
Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.