Zaburi 128:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA akubariki toka Sayuni; Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu akubariki kutoka Siyoni! Uione fanaka ya Yerusalemu, siku zote za maisha yako. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu akubariki kutoka Siyoni! Uione fanaka ya Yerusalemu, siku zote za maisha yako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu akubariki kutoka Siyoni! Uione fanaka ya Yerusalemu, siku zote za maisha yako. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu na akubariki kutoka Sayuni siku zote za maisha yako, na uone mafanikio ya Yerusalemu, Neno: Maandiko Matakatifu bwana na akubariki kutoka Sayuni siku zote za maisha yako, na uone mafanikio ya Yerusalemu, BIBLIA KISWAHILI BWANA akubariki toka Sayuni; Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako; |
Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa BWANA, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la BWANA katika Yerusalemu.
Angalia Sayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yako yatauona Yerusalemu umekuwa makao ya raha; hema isiyotikisika; vigingi vyake havitang'olewa, wala kamba zake hazitakatika.
Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;