Akaona haitoshi kumtia mikono Mordekai peke yake; maana wamemjulisha kabila lake Mordekai; kwa hiyo Hamani alitaka kuwaangamiza Wayahudi wote waliokuwa wakikaa katika ufalme wote mzima wa Ahasuero, yaani, watu wake Mordekai.
Zaburi 124:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Papo hapo wangalitumeza hai, Hasira yao ilipowaka juu yetu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema hakika tungalimezwa tukiwa hai, wakati hasira zao zilipotuwakia. Biblia Habari Njema - BHND hakika tungalimezwa tukiwa hai, wakati hasira zao zilipotuwakia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza hakika tungalimezwa tukiwa hai, wakati hasira zao zilipotuwakia. Neno: Bibilia Takatifu hasira yao ilipowaka dhidi yetu, wangetumeza tukiwa hai, Neno: Maandiko Matakatifu wakati hasira yao ilipowaka dhidi yetu, wangalitumeza tungali hai, BIBLIA KISWAHILI Papo hapo wangalitumeza hai, Hasira yao ilipowaka juu yetu. |
Akaona haitoshi kumtia mikono Mordekai peke yake; maana wamemjulisha kabila lake Mordekai; kwa hiyo Hamani alitaka kuwaangamiza Wayahudi wote waliokuwa wakikaa katika ufalme wote mzima wa Ahasuero, yaani, watu wake Mordekai.
Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka.
Atanitumia msaada toka mbinguni na kuniokoa, Atawaaibisha wale wanaotaka kunishambulia. Mungu atazituma Fadhili zake na kweli yake.
Walisema mioyoni mwao, Na tuwaangamize kabisa; Mahali penye mikutano ya Mungu Wamepachoma moto katika nchi pia.
Wamesema, Njoni, tuwakatilie mbali wasiwe taifa, Na jina la Israeli halitakumbukwa tena.
Nebukadneza, mfalme wa Babeli, amenila, ameniponda, amenifanya kuwa chombo kitupu; amenimeza kama joka, amelijaza tumbo lake vitu vyangu vya anasa; amenitupa
Ndipo Nebukadneza akajaa ghadhabu, na sura ya uso wake ikabadilika juu ya Shadraka, na Meshaki, na Abednego, basi akatoa amri watie moto ile tanuri mara saba kuliko desturi yake ya kutiwa moto.
BWANA akaweka tayari samaki mkubwa ili ammeze Yona, naye Yona akawa ndani ya tumbo la samaki yule muda wa siku tatu, mchana na usiku.
Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale majusi, alighadhibika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wa kiume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake kote, kuanzia wenye miaka miwili na chini yake, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale majusi.
akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, wanaume kwa wanawake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.