Zamani za kale, hapo Sauli alipokuwa mfalme juu yetu, wewe ndiwe uliyewaongoza Israeli wakitoka nje kwenda, na kurudi vitani. Naye BWANA akakuambia, Wewe utawalisha watu wangu Israeli, nawe utakuwa mkuu juu ya Israeli.
Zaburi 121:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu atakulinda katika shughuli zako zote tangu sasa na hata milele. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu atakulinda katika shughuli zako zote tangu sasa na hata milele. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu atakulinda katika shughuli zako zote tangu sasa na hata milele. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu atakulinda unapoingia na unapotoka, tangu sasa na hata milele. Neno: Maandiko Matakatifu bwana atakulinda unapoingia na unapotoka, tangu sasa na hata milele. BIBLIA KISWAHILI BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele. |
Zamani za kale, hapo Sauli alipokuwa mfalme juu yetu, wewe ndiwe uliyewaongoza Israeli wakitoka nje kwenda, na kurudi vitani. Naye BWANA akakuambia, Wewe utawalisha watu wangu Israeli, nawe utakuwa mkuu juu ya Israeli.
Ndipo nikaamuru kufunga, hapo penye mto Ahava, ili tupate kujinyenyekeza mbele za Mungu, na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili yetu sisi wenyewe, na kwa ajili ya watoto wetu, na kwa mali yetu yote.
Ndipo tukasafiri toka mtoni Ahava siku ya kumi na mbili ya mwezi wa kwanza, ili kwenda Yerusalemu; na mkono wa Mungu ulikuwa pamoja nasi, akatuokoa na mkono wa adui, na mtu mwenye kutuvizia njiani.
Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele.