Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.
Zaburi 121:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu atakukinga na baya lolote; atayalinda salama maisha yako. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu atakukinga na baya lolote; atayalinda salama maisha yako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu atakukinga na baya lolote; atayalinda salama maisha yako. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu atakukinga na madhara yote, atayalinda maisha yako, Neno: Maandiko Matakatifu bwana atakukinga na madhara yote, atayalinda maisha yako, BIBLIA KISWAHILI BWANA atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako. |
Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.
Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibariki kweli kweli, na kuipanua mipaka yangu, na mkono wako ukawa pamoja nami, nawe ungenilinda nisipatwe na maovu wala madhara! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
BWANA atamlinda na kumhifadhi hai, Naye atafanikiwa katika nchi; Wala usimtie katika hali wamtakiayo adui zake.
Enyi mmpendao BWANA, uchukieni uovu; Huwalinda nafsi zao watauwa wake, Na kuwaokoa na mkono wa wasio haki.
Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.
Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike katika ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.