Zaburi 121:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA ndiye mlinzi wako; BWANA ni uvuli katika mkono wako wa kulia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu ni mlinzi wako; yuko upande wako wa kulia kukukinga. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu ni mlinzi wako; yuko upande wako wa kulia kukukinga. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu ni mlinzi wako; yuko upande wako wa kulia kukukinga. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu anakulinda, Mwenyezi Mungu ni uvuli wako mkono wako wa kuume, Neno: Maandiko Matakatifu bwana anakulinda, bwana ni uvuli wako mkono wako wa kuume, BIBLIA KISWAHILI BWANA ndiye mlinzi wako; BWANA ni uvuli katika mkono wako wa kulia. |
BWANA naye akawatangulia mchana ndani ya wingu mfano wa nguzo, ili awaongoze njia; na usiku, ndani ya moto mfano wa nguzo, ili kuwapa nuru; wapate kusafiri mchana na usiku;
Maana umekuwa ngome ya maskini, Ngome ya mhitaji katika dhiki yake, Mahali pa kukimbilia wakati wa tufani, Na kivuli wakati wa joto; Wakati kishindo cha watu wakatili kilipokuwa, Kama dhoruba ipigayo ukuta.
Na mwanadamu atakuwa kama mahali pa kujificha na upepo, na mahali pa kujisitiri na dhoruba; kama mito ya maji mahali pakavu, kama kivuli cha mwamba mkubwa katika nchi yenye uchovu.
Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku awakusanyavyo pamoja vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!