BWANA asipoijenga nyumba Waijengao wanafanya kazi bure. BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye anakesha bure.
Zaburi 121:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hatauacha mguu wako usogezwe; Akulindaye hatasinzia; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hatakuacha uanguke; mlinzi wako hasinzii. Biblia Habari Njema - BHND Hatakuacha uanguke; mlinzi wako hasinzii. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hatakuacha uanguke; mlinzi wako hasinzii. Neno: Bibilia Takatifu Hatauacha mguu wako uteleze, yeye akulindaye hatasinzia, Neno: Maandiko Matakatifu Hatauacha mguu wako uteleze, yeye akulindaye hatasinzia, BIBLIA KISWAHILI Hatauacha mguu wako usogezwe; Akulindaye hatasinzia; |
BWANA asipoijenga nyumba Waijengao wanafanya kazi bure. BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye anakesha bure.
BWANA atamlinda na kumhifadhi hai, Naye atafanikiwa katika nchi; Wala usimtie katika hali wamtakiayo adui zake.
Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.
Mimi, BWANA, nililinda, Nitalitia maji kila dakika, Asije mtu akaliharibu; Usiku na mchana nitalilinda.
Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani ili mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.
Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda;