Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.
Zaburi 120:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa muda mrefu nimeishi, Pamoja na watu wanaoichukia amani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nimeishi muda mrefu mno kati ya watu wanaochukia amani! Biblia Habari Njema - BHND Nimeishi muda mrefu mno kati ya watu wanaochukia amani! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nimeishi muda mrefu mno kati ya watu wanaochukia amani! Neno: Bibilia Takatifu Nimeishi muda mrefu mno miongoni mwa wale wanaochukia amani. Neno: Maandiko Matakatifu Nimeishi muda mrefu mno miongoni mwa wale wanaochukia amani. BIBLIA KISWAHILI Kwa muda mrefu nimeishi, Pamoja na watu wanaoichukia amani. |
Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.
Na wewe, mwanadamu, usiwaogope hao, wala usiyaogope maneno yao, ijapokuwa miiba na michongoma inakuzunguka, nawe unakaa katikati ya nge; usiyaogope maneno yao, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba yenye kuasi.
Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwamwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.