Wao ni wana wa wapumbavu, naam, watoto wa wahuni; Walifukuzwa kwa mijeledi watoke katika nchi.
Zaburi 12:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wasio haki hutembea pande zote, Huku ufisadi ukitukuka kati ya wanadamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waovu wanazunguka kila mahali; upotovu unatukuzwa kati ya watu. Biblia Habari Njema - BHND Waovu wanazunguka kila mahali; upotovu unatukuzwa kati ya watu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waovu wanazunguka kila mahali; upotovu unatukuzwa kati ya watu. Neno: Bibilia Takatifu Watu waovu huenda wakiringa kila mahali wakati yule aliye mbaya sana ndiye anayeheshimiwa miongoni mwa watu. Neno: Maandiko Matakatifu Watu waovu huenda wakiringa kila mahali wakati ambapo yule aliye mbaya sana ndiye anayeheshimiwa miongoni mwa watu. BIBLIA KISWAHILI Wasio haki hutembea pande zote, Huku ufisadi ukitukuka kati ya wanadamu. |
Wao ni wana wa wapumbavu, naam, watoto wa wahuni; Walifukuzwa kwa mijeledi watoke katika nchi.
Kisha badala yake atasimama mmoja, mtu astahiliye kudharauliwa, ambaye hawakumpa heshima ya ufalme; naye atakuja wakati wa amani, naye ataupata ufalme kwa kujipendekeza.
Kwa maana amri za Omri ndizo zishikwazo, na matendo yote ya nyumba ya Ahabu, nanyi mnakwenda katika mashauri yao; ili nikufanye kuwa ukiwa, na wenyeji waliomo humo kuwa zomeo; nanyi mtayachukua matukano waliyotukanwa watu wangu.