Lakini yeye huokoa na upanga wa kinywa chao, Hata kumwokoa mhitaji na mkono wake aliye hodari.
Zaburi 12:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Mwenyezi-Mungu asema: “Kwa sababu maskini wanadhulumiwa, na wahitaji wanapiga kite, sasa naja, nami nitawapa usalama wanaoutazamia.” Biblia Habari Njema - BHND Lakini Mwenyezi-Mungu asema: “Kwa sababu maskini wanadhulumiwa, na wahitaji wanapiga kite, sasa naja, nami nitawapa usalama wanaoutazamia.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Mwenyezi-Mungu asema: “Kwa sababu maskini wanadhulumiwa, na wahitaji wanapiga kite, sasa naja, nami nitawapa usalama wanaoutazamia.” Neno: Bibilia Takatifu “Kwa sababu wanyonge wanaonewa, na wahitaji wanalia kwa uchungu, nitainuka sasa,” asema Mwenyezi Mungu. “Nitawalinda kutokana na wale wenye nia mbaya juu yao.” Neno: Maandiko Matakatifu “Kwa sababu ya uonevu wa wanyonge na kulia kwa uchungu kwa wahitaji, nitainuka sasa,” asema bwana. “Nitawalinda kutokana na wale wenye nia mbaya juu yao.” BIBLIA KISWAHILI Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya. |
Lakini yeye huokoa na upanga wa kinywa chao, Hata kumwokoa mhitaji na mkono wake aliye hodari.
Njia zake ni thabiti kila wakati. Hukumu zako ziko juu asizione, Adui zake wote awakaripia.
Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako Ulizowawekea wakuchao; Ulizowatendea wakukimbiliao Mbele ya wanadamu!
Farao akasema, BWANA ni nani, hata niisikilize sauti yake, na kuwapa Israeli ruhusa waende zao? Mimi simjui BWANA, wala sitawapa Israeli ruhusa waende zao.
Kisha nikarudi na kuona udhalimu wote unaotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, lakini wale walikuwa hawana mfariji.
Ujapokuwa unaona maskini kuonewa, na hukumu na haki kuondolewa kwa jeuri katika jimbo, usilistaajabie jambo hilo; kwa sababu, Aliye Juu kuliko walio juu huangalia; Tena wako walio juu kupita hao.
Nayo itakuwa ishara na ushuhuda kwa BWANA wa majeshi katika nchi ya Misri; kwa maana watamlilia BWANA kwa sababu ya watu wawaoneao, naye atawapelekea mwokozi wa kuwatetea, naye atawaokoa.
Kwa habari za yule baba yake, kwa sababu aliwaonea watu kwa ukali mwingi, na kumnyang'anya ndugu yake mali yake kwa nguvu; na kuyatenda yasiyo mema kati ya watu wake, tazama, atakufa katika uovu wake.
Wao hurudi, lakini si kwake Aliye Juu; wamekuwa kama upinde usiotumainika; wakuu wao wataanguka kwa upanga, kwa sababu ya ujeuri wa ndimi zao; na kwa sababu hiyo watachekwa katika nchi ya Misri.
Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliokosa kuwalipa kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi.
Nao wakaiondoa hiyo miungu ya kigeni iliyokuwa kati yao, nao wakamtumikia BWANA; na roho yake ilihuzunika kwa sababu ya msiba wa Israeli.