Sasa, Ee Mungu wa Israeli, nakusihi, ulithibitishe neno lako, ulilomwambia mtumishi wako, Daudi, baba yangu.
Zaburi 119:38 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Umthibitishie mtumishi wako ahadi yako, Iliyo ya wanaokucha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Unitimizie mimi mtumishi wako ahadi yako; ahadi unayowapa wale wanaokuheshimu. Biblia Habari Njema - BHND Unitimizie mimi mtumishi wako ahadi yako; ahadi unayowapa wale wanaokuheshimu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Unitimizie mimi mtumishi wako ahadi yako; ahadi unayowapa wale wanaokuheshimu. Neno: Bibilia Takatifu Mtimizie mtumishi wako ahadi yako, ili upate kuogopwa. Neno: Maandiko Matakatifu Mtimizie mtumishi wako ahadi yako, ili upate kuogopwa. BIBLIA KISWAHILI Umthibitishie mtumishi wako ahadi yako, Inayohusu wanaokucha. |
Sasa, Ee Mungu wa Israeli, nakusihi, ulithibitishe neno lako, ulilomwambia mtumishi wako, Daudi, baba yangu.
Maana, kama mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, Ndivyo fadhili zake zilivyo kuu kwa wamchao.
Bali fadhili za BWANA ni kwa wamchao Tangu milele hata milele, Na haki yake ni kwa vizazi vyote;
Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi.