Zaburi 119:165 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wana amani nyingi waipendao sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wapendao sheria yako wana amani kuu; hakuna kinachoweza kuwaangusha. Biblia Habari Njema - BHND Wapendao sheria yako wana amani kuu; hakuna kinachoweza kuwaangusha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wapendao sheria yako wana amani kuu; hakuna kinachoweza kuwaangusha. Neno: Bibilia Takatifu Wanaopenda sheria yako wana amani tele, wala hakuna kitu kinachoweza kuwakwaza. Neno: Maandiko Matakatifu Wanaopenda sheria yako wana amani tele, wala hakuna kitu kinachoweza kuwakwaza. BIBLIA KISWAHILI Wana amani nyingi waipendao sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza. |
Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.
Kwa sababu hiyo neno la BWANA kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo; ili waende na kuanguka nyuma, na kuvunjwa, na kunaswa, na kuchukuliwa.
Naye atasema, Tutieni, tutieni, Itengenezeni njia, Ondoeni kila kizuizi Katika njia ya watu wangu.
lakini hana mizizi ndani yake, bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara huchukizwa.
Kwa maana watatokea Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, ikiwezekana, hata walio wateule.
Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.
Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.