Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu chochote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nimkosee Mungu?
Zaburi 119:161 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wakuu wameniudhi bure, Ila moyo wangu unakaa kwa kicho cha maneno yako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakuu wanidhulumu bila kisa, lakini mimi naheshimu maneno yako kwa moyo wote. Biblia Habari Njema - BHND Wakuu wanidhulumu bila kisa, lakini mimi naheshimu maneno yako kwa moyo wote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakuu wanidhulumu bila kisa, lakini mimi naheshimu maneno yako kwa moyo wote. Neno: Bibilia Takatifu Watawala wamenitesa bila sababu, lakini moyo wangu unatetemeka kwa neno lako. Neno: Maandiko Matakatifu Watawala wamenitesa bila sababu, lakini moyo wangu unatetemeka kwa neno lako. BIBLIA KISWAHILI Wakuu wameniudhi bure, Ila moyo wangu unakaa kwa kicho cha maneno yako. |
Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu chochote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nimkosee Mungu?
kwa kuwa moyo wako ulikuwa mwororo, nawe ukajinyenyekeza mbele za BWANA, hapo ulipoyasikia maneno niliyoyanena juu ya mahali hapa, na juu ya wenyeji wake, ya kwamba watakuwa ukiwa na laana, nawe ulizirarua nguo zako, ukalia mbele zangu; basi, mimi nami nimekusikia wewe, asema BWANA.
Lakini watawala wa kwanza walionitangulia, wakawalemea watu, wakawatwalia chakula na mvinyo, zaidi ya shekeli arubaini za fedha; tena hata watumishi wao nao wakawatawala watu; lakini mimi sikufanya hivyo, kwa kuwa nilimcha Mungu.
Kwani msiba utokao kwa Mungu ulikuwa na kitisho kwangu, Na kwa sababu ya ukuu wake sikuweza kufanya neno.
Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.
Je! Mimi nina haja ya watu wenye wazimu, hata mmemleta kiumbe huyu ili aoneshe wazimu wake machoni pangu? Je! Huyu ataingia nyumbani mwangu?
Akasema, Bwana wangu ananiwinda mimi mtumishi wake kwa sababu gani? Nimefanya nini mimi? Ni uovu gani nilio nao mkononi mwangu?