Zaburi 119:157 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wanaonifuatia na watesi wangu ni wengi, Lakini mimi sikiuki shuhuda zako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maadui na wadhalimu wangu ni wengi, lakini mimi sikiuki maamuzi yako. Biblia Habari Njema - BHND Maadui na wadhalimu wangu ni wengi, lakini mimi sikiuki maamuzi yako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maadui na wadhalimu wangu ni wengi, lakini mimi sikiuki maamuzi yako. Neno: Bibilia Takatifu Adui wanaonitesa ni wengi, lakini mimi sitaziacha sheria zako. Neno: Maandiko Matakatifu Adui wanaonitesa ni wengi, lakini mimi sitaziacha sheria zako. BIBLIA KISWAHILI Wanaonifuatia na watesi wangu ni wengi, Lakini mimi sikujiepusha na shuhuda zako. |
Kwa maana mbwa wamenizunguka; Kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenidunga mikono na miguu.
Hatazimia, wala hatakata tamaa, hata atakapoweka hukumu duniani; na visiwa vitaingojea sheria yake.
Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.
Basi alipokuwa katika kusema, tazama, Yuda, mmoja wa wale Kumi na Wawili akaja, na pamoja naye kundi kubwa wenye panga na marungu, wametoka kwa wakuu wa makuhani na wazee wa watu.
Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,
Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mnajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.