Zaburi 119:123 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Macho yangu yanafifia kwa kuungojea wokovu wako, Na kutimizwa kwa ahadi yako ya haki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Macho yangu yanafifia nikingojea uniokoe, nikingojea utimize uliyoahidi. Biblia Habari Njema - BHND Macho yangu yanafifia nikingojea uniokoe, nikingojea utimize uliyoahidi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Macho yangu yanafifia nikingojea uniokoe, nikingojea utimize uliyoahidi. Neno: Bibilia Takatifu Macho yangu yamefifia, yakitazamia wokovu wako, na kuitazamia ahadi yako ya kweli. Neno: Maandiko Matakatifu Macho yangu yamefifia, yakitazamia wokovu wako, na kuitazamia ahadi yako ya kweli. BIBLIA KISWAHILI Macho yangu yanafifia kwa kuungojea wokovu wako, Na kutimizwa kwa ahadi yako ya haki. |
Nafsi yangu inamngoja Bwana, Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi, Naam, walinzi waingojao asubuhi.
Ee BWANA, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni.
Nimechoka kwa kulia kwangu, Koo yangu imekauka. Macho yangu yamedhoofika Kwa kumngoja Mungu wangu.
Macho yetu yamechoka Kwa kuutazamia bure msaada wetu; Katika kungoja kwetu tumengojea taifa Lisiloweza kutuokoa.