Ikawa, mfalme alipokwisha kuyasikia maneno ya kitabu hicho cha torati, alirarua nguo zake.
Zaburi 119:120 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mwili wangu unatetemeka kwa kukucha Wewe, Nami ninaziogopa hukumu zako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Natetemeka kwa kukuogopa wewe; nimejaa hofu kwa sababu ya hukumu zako. Biblia Habari Njema - BHND Natetemeka kwa kukuogopa wewe; nimejaa hofu kwa sababu ya hukumu zako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Natetemeka kwa kukuogopa wewe; nimejaa hofu kwa sababu ya hukumu zako. Neno: Bibilia Takatifu Mwili wangu unatetemeka kwa kukuogopa wewe, ninaziogopa sheria zako. Neno: Maandiko Matakatifu Mwili wangu unatetemeka kwa kukuogopa wewe, ninaziogopa sheria zako. BIBLIA KISWAHILI Mwili wangu unatetemeka kwa kukucha Wewe, Nami ninaziogopa hukumu zako. |
Ikawa, mfalme alipokwisha kuyasikia maneno ya kitabu hicho cha torati, alirarua nguo zake.
Na wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi. Hao ndio wana wa Walawi, kwa kufuata koo za baba zao.
Nendeni, mkamwulize BWANA kwa ajili yangu, na kwa hao waliosalia wa Israeli na wa Yuda, kuhusu habari za maneno ya kitabu kilichoonekana; maana ghadhabu ya BWANA ni nyingi iliyomwagika juu yetu, kwa sababu baba zetu hawakulishika neno la BWANA, kutenda sawasawa na yote yaliyoandikwa kitabuni humo.
kwa kuwa moyo wako ulikuwa mwororo, nawe umejinyenyekeza mbele ya Mungu, uliposikia maneno yake juu ya mahali hapa, na juu ya wakazi wake, ukajinyenyekeza mbele zangu, na kuyararua mavazi yako, na kulia mbele zangu; mimi nami nimekusikia, asema BWANA.
Kwani msiba utokao kwa Mungu ulikuwa na kitisho kwangu, Na kwa sababu ya ukuu wake sikuweza kufanya neno.
Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.
Lisikilizeni neno la BWANA, ninyi mtetemekao kwa sababu ya neno lake; Ndugu zenu wawachukiao ninyi, waliowatupa kwa ajili ya jina langu, wamesema, Na atukuzwe BWANA, tupate kuiona furaha yenu; lakini watatahayarika.
Nikasikia, na tumbo langu likatetemeka, Midomo yangu ikatikisika kwa sauti ile; Ubovu ukaingia mifupani mwangu, Nikatetemeka katika mahali pangu; Ili nipate kuingoja ile siku ya dhiki, Kundi lao washambuliao wakweapo juu ya watu.
Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.
Na hayo yaliyoonekana jinsi yalivyokuwa ya kutisha, hata Musa akasema, Nimeshikwa na hofu na kutetemeka.
Nao watu wa Beth-shemeshi wakasema, Ni nani awezaye kusimama mbele za BWANA, huyu Mungu mtakatifu? Naye atapanda kwenda kwa nani kutoka kwetu?