Zaburi 119:117 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Unisaidie nami nitakuwa salama, Nami nitaziangalia amri zako daima. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Unitegemeze, niwe salama; niwe daima msikivu kwa masharti yako. Biblia Habari Njema - BHND Unitegemeze, niwe salama; niwe daima msikivu kwa masharti yako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Unitegemeze, niwe salama; niwe daima msikivu kwa masharti yako. Neno: Bibilia Takatifu Nitegemeze, nami nitaokolewa, nami daima nitayaheshimu maagizo yako. Neno: Maandiko Matakatifu Nitegemeze, nami nitaokolewa, nami daima nitayaheshimu maagizo yako. BIBLIA KISWAHILI Unisaidie nami nitakuwa salama, Nami nitaziangalia amri zako daima. |
Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa, Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu, Ninakusifu Wewe daima.
Kwa maana mimi, BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kulia, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia.
Wewe u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha.
Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani ili mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.
Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu;