Zaburi 119:116 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Unitegemeze kulingana na ahadi yako, nikaishi, Wala usiniache niyaaibikie matumaini yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uniimarishe ulivyoahidi, nami nitaishi; usikubali niaibike katika tumaini langu. Biblia Habari Njema - BHND Uniimarishe ulivyoahidi, nami nitaishi; usikubali niaibike katika tumaini langu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uniimarishe ulivyoahidi, nami nitaishi; usikubali niaibike katika tumaini langu. Neno: Bibilia Takatifu Nihifadhi sawasawa na ahadi yako, nami nitaishi; usiache matumaini yangu yakavunjwa. Neno: Maandiko Matakatifu Nihifadhi sawasawa na ahadi yako, nami nitaishi; usiache matumaini yangu yakavunjwa. BIBLIA KISWAHILI Unitegemeze kulingana na ahadi yako, nikaishi, Wala usiniache niyaaibikie matumaini yangu. |
usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.
Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu.
Bali Israeli wataokolewa na BWANA kwa wokovu wa milele; ninyi hamtatahayarika, wala kufadhaika, milele na milele.
na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.
Kwa kuwa imeandikwa katika Maandiko: Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.