Zaburi 118:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu yuko nami, siogopi kitu; binadamu ataweza kunifanya nini? Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu yuko nami, siogopi kitu; binadamu ataweza kunifanya nini? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu yuko nami, siogopi kitu; binadamu ataweza kunifanya nini? Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu yuko pamoja nami, sitaogopa. Mwanadamu anaweza kunitenda nini? Neno: Maandiko Matakatifu bwana yuko pamoja nami, sitaogopa. Mwanadamu anaweza kunitenda nini? BIBLIA KISWAHILI BWANA yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini? |
Naam, nijapopita kati ya bonde la kivuli cha mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake. Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwenye mwili atanitenda nini?
Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo. Neno hili najua kuwa MUNGU yu upande wangu;
Ni nani atakayesimama Kwa ajili yangu juu ya wabaya? Ni nani atakayenisaidia Juu yao wafanyao maovu?
Mimi, naam, mimi, ndimi niwafarijiye; wewe u nani hata ukamwogopa mtu atakayekufa, na mwanadamu atakayefanywa kuwa kama majani?
Lakini BWANA yuko pamoja nami, mfano wa shujaa mwenye kutisha; kwa hiyo hao wanaonionea watajikwaa, wala hawatashinda; watatahayarika sana. Kwa sababu hawatafaulu wataona aibu ya milele, ambayo haitasahauliwa kamwe.
Basi Sauli na Israeli wote waliposikia maneno hayo ya Mfilisti, wakafadhaika na kuogopa sana.
Daudi akasema, BWANA aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Nenda, na BWANA atakuwa pamoja nawe.