Zaburi 118:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la BWANA; Tumewabariki toka nyumbani mwa BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Mwenyezi-Mungu! Twawabariki kutoka nyumbani mwa Mwenyezi-Mungu Biblia Habari Njema - BHND Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Mwenyezi-Mungu! Twawabariki kutoka nyumbani mwa Mwenyezi-Mungu Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Mwenyezi-Mungu! Twawabariki kutoka nyumbani mwa Mwenyezi-Mungu Neno: Bibilia Takatifu Heri yule ajaye kwa jina la Mwenyezi Mungu. Kutoka nyumba ya Mwenyezi Mungu tunakubariki. Neno: Maandiko Matakatifu Heri yule ajaye kwa jina la bwana. Kutoka nyumba ya bwana tunakubariki. BIBLIA KISWAHILI Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la BWANA; Tumewabariki toka nyumbani mwa BWANA. |
Nani wewe, Ee mlima mkubwa? Mbele ya Zerubabeli utakuwa nchi tambarare; naye atalileta lile jiwe la kuwekwa juu kabisa pamoja na vigelegele vya, Neema, neema, ilikalie.
Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni.
Kwa maana nawaambia, Hamtaniona kamwe tangu sasa, hadi mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Angalieni, mmeachiwa nyumba yenu! Nami nawaambia, Hamtaniona tena kamwe, hadi mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
wakasema, Ndiye mbarikiwa Mfalme ajaye kwa jina la Bwana; amani mbinguni, na utukufu huko juu.
wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana! Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli!