BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
Zaburi 118:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA ni nguvu zangu na wimbo wangu, Naye amekuwa wokovu wangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu ni nguvu yangu kuu; yeye mwenyewe ndiye wokovu wangu. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu ni nguvu yangu kuu; yeye mwenyewe ndiye wokovu wangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu ni nguvu yangu kuu; yeye mwenyewe ndiye wokovu wangu. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu ni nguvu yangu na wimbo wangu, yeye amefanyika wokovu wangu. Neno: Maandiko Matakatifu bwana ni nguvu yangu na wimbo wangu, yeye amefanyika wokovu wangu. BIBLIA KISWAHILI BWANA ni nguvu zangu na wimbo wangu, Naye amekuwa wokovu wangu. |
BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?
Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu.
Bali Israeli wataokolewa na BWANA kwa wokovu wa milele; ninyi hamtatahayarika, wala kufadhaika, milele na milele.