Zaburi 116:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ee nafsi yangu, urudi pumzikoni mwako, Kwa kuwa BWANA amekutendea ukarimu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uwe na utulivu mkuu, ee nafsi yangu, maana Mwenyezi-Mungu amenitendea mema. Biblia Habari Njema - BHND Uwe na utulivu mkuu, ee nafsi yangu, maana Mwenyezi-Mungu amenitendea mema. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uwe na utulivu mkuu, ee nafsi yangu, maana Mwenyezi-Mungu amenitendea mema. Neno: Bibilia Takatifu Ee nafsi yangu, tulia tena, kwa kuwa Mwenyezi Mungu amekuwa mwema kwako. Neno: Maandiko Matakatifu Ee nafsi yangu, tulia tena, kwa kuwa bwana amekuwa mwema kwako. BIBLIA KISWAHILI Ee nafsi yangu, urudi rahani mwako, Kwa kuwa BWANA amekutendea ukarimu. |
Kwa sababu hiyo usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu, asema BWANA; wala usifadhaike, Ee Israeli; kwa maana, tazama, nitakuokoa toka mbali, na wazao wako toka nchi ya uhamisho wao; na Yakobo atarudi, naye atatulia na kustarehe, wala hapana mtu atakayemtia hofu.
BWANA asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, Iko wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo.
Naye atawafuata wapenzi wake, lakini hatawapata; atawatafuta, lakini hatawaona; ndipo atakaposema, Nitakwenda nikamrudie mume wangu wa kwanza; kwa maana hali yangu ya zamani ilikuwa njema kuliko hali yangu ya sasa.