Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana.
Zaburi 115:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Enyi mlango wa Haruni, mtumainini BWANA; Yeye ni msaada wao na ngao yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Enyi wazawa wa Aroni, mtumainieni Mwenyezi-Mungu; yeye ndiye msaada wenu na ngao yenu. Biblia Habari Njema - BHND Enyi wazawa wa Aroni, mtumainieni Mwenyezi-Mungu; yeye ndiye msaada wenu na ngao yenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Enyi wazawa wa Aroni, mtumainieni Mwenyezi-Mungu; yeye ndiye msaada wenu na ngao yenu. Neno: Bibilia Takatifu Ee nyumba ya Haruni, mtumainini Mwenyezi Mungu, yeye ni msaada na ngao yao. Neno: Maandiko Matakatifu Ee nyumba ya Haruni, mtumainini bwana, yeye ni msaada na ngao yao. BIBLIA KISWAHILI Enyi mlango wa Haruni, mtumainini BWANA; Yeye ni msaada wao na ngao yao. |
Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana.
Nawe umlete Haruni ndugu yako karibu nami, na wanawe pamoja naye, miongoni mwa wana wa Israeli, ili anitumikie katika kazi ya ukuhani. Haruni, na Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari, wana wa Haruni.
viwe ukumbusho kwa wana wa Israeli, ili mgeni yeyote asiye wa kizazi cha Haruni, asikaribie kufukiza uvumba mbele za BWANA; asiwe mfano wa Kora, na mkutano wake; kama BWANA alivyonena naye, kwa kupitia kwa Musa.
kisha akanena na Kora na mkutano wake wote, akawaambia, Asubuhi BWANA ataonesha ni kina nani walio wake, kisha ni nani aliye mtakatifu, tena ni nani atakayemkaribisha kwake; maana, yeye atakayemchagua ndiye atakayemsongeza kwake.
Nawe na wanao pamoja nawe mtautunza ukuhani wenu, kwa ajili ya kila kitu cha madhabahu, na kwa ajili ya vile vilivyomo ndani ya pazia, nanyi mtatumika. Nawapeni ukuhani kuwa utumishi wa kipawa; na mgeni akaribiaye atauawa.