Ndipo nchi iliyotikisika na kutetemeka, Misingi ya milima ikatingizika; Ikatikisika kwa sababu alikuwa na ghadhabu.
Zaburi 114:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Milima iliruka kama kondoo dume, Vilima kama wana-kondoo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Milima ilirukaruka kama kondoo dume; vilima vikaruka kama wanakondoo! Biblia Habari Njema - BHND Milima ilirukaruka kama kondoo dume; vilima vikaruka kama wanakondoo! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Milima ilirukaruka kama kondoo dume; vilima vikaruka kama wanakondoo! Neno: Bibilia Takatifu milima ilirukaruka kama kondoo dume, vilima kama wana-kondoo. Neno: Maandiko Matakatifu milima ilirukaruka kama kondoo dume, vilima kama wana-kondoo. BIBLIA KISWAHILI Milima iliruka kama kondoo dume, Vilima kama wana-kondoo. |
Ndipo nchi iliyotikisika na kutetemeka, Misingi ya milima ikatingizika; Ikatikisika kwa sababu alikuwa na ghadhabu.
Kweli, watu wote hupita kama kivuli; Wao hujisumbua bure tu; Wanajirundikia mali wala hawajui ni nani atakayeirithi.
Enyi milima mirefu, kwani kuutazama kwa wivu Mlima alioutamani Mungu akae juu yake? Naam, BWANA atakaa juu yake milele.
Mlima wa Sinai wote pia ukatoa moshi, kwa sababu BWANA alishuka katika moto; na ule moshi wake ukapanda juu kama moshi wa tanuri, mlima wote ukatetemeka sana.
Watu wote wakaona umeme na ngurumo na sauti ya baragumu, na ule mlima kutoka moshi; na watu walipoona hayo wakatetemeka, wakasimama mbali.
Milima hutetema mbele zake, navyo vilima huyeyuka; nayo dunia huinuliwa mbele za uso wake, naam, dunia na wote wakaao ndani yake.
Akasimama na kuitikisa dunia; Akatazama, mataifa yakatetemeka; Na milima ya zamani ikatawanyika; Vilima vya kale vikainama; Miendo yake ilikuwa kama siku za kale.
Je! BWANA aliikasirikia mito? Je! Hasira yako ilikuwa juu ya mito, Au ghadhabu yako juu ya bahari, Hata ukapanda farasi wako, Katika magari yako ya wokovu?
Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.