Kwa kuwa mimi nilikuinua kutoka katika mavumbi, na kukufanya uwe mkuu juu ya watu wangu Israeli; nawe umeiendea njia ya Yeroboamu, na kuwakosesha watu wangu Israeli, hata wanighadhibishe kwa makosa yao;
Zaburi 113:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Na kumpandisha maskini kutoka jaani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Humwinua fukara kutoka mavumbini; humnyanyua maskini kutoka unyonge wake, Biblia Habari Njema - BHND Humwinua fukara kutoka mavumbini; humnyanyua maskini kutoka unyonge wake, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Humwinua fukara kutoka mavumbini; humnyanyua maskini kutoka unyonge wake, Neno: Bibilia Takatifu Huwainua maskini kutoka mavumbini, na kuwanyanyua wahitaji kutoka lundo la majivu, Neno: Maandiko Matakatifu Huwainua maskini kutoka mavumbini, na kuwanyanyua wahitaji kutoka kwenye jalala, BIBLIA KISWAHILI Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Na kumpandisha maskini kutoka jaani. |
Kwa kuwa mimi nilikuinua kutoka katika mavumbi, na kukufanya uwe mkuu juu ya watu wangu Israeli; nawe umeiendea njia ya Yeroboamu, na kuwakosesha watu wangu Israeli, hata wanighadhibishe kwa makosa yao;
Lakini alimwinua mhitaji juu mbali na mateso, Na kuwaongeza jamaa zao kama kundi la kondoo.
Nguvu zangu zimekauka kama gae, Ulimi wangu waambatana na taya zangu; Unaniweka katika mavumbi ya mauti
Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.
Na miti yote ya mashamba itajua ya kuwa mimi, BWANA, nimeushusha chini mti mrefu, na kuuinua mti mfupi, na kuukausha mti mbichi, na kuusitawisha mti mkavu; mimi, BWANA, nimenena, nami nimelitenda jambo hili.
Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?
Na mfalme wa Israeli ametoka ili kumfuatia nani? Unamwinda nani? Ni kuwinda mbwa mfu, au kiroboto.